Baruwa ya Mzungoko - Mwisho wa mwaka 2018
Kwa moyo wangu wote nina wasalimu wandugu na wa dada ulimwenguni pote katika Jina tukufu la BWANA wetu Yesu Kristo na andiko kutoka 1. Thes 3:13:
“Apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake BWANA wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote!“
Hapo kwa sura ifuatayo ya shahiri 13 hadi 17, Mtume aliionyesha namna itakavyo tendeka wakati wa kurudi kwake. “…kwa kuwa twa waambieni haya kwa Neno la BWANA, kwamba sisi tulio hai, tutakao salia hata wakati wakuja kwake BWANA, hakika hatuta watangulia wao walio kwisha kulala mauti.
Kwa sababu BWANA mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao walio kufa katika Kristo wata fufuliwa kwanza; Kiisha sisi tulio hai, tulio salia, tutanya kuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumulaki BWANA hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na BWANA milele“ (1. Thes. 4:15-17). Mwaliko, sauti, na sauti ya tarumbeta itasikilika wakati wa ufufuko, kubadilishwa na kunyakuliwa.
Sasa kwa mwisho wa wakati wa neema, kelele ya usiku wa manane ina sikilikana kuita waamini wote: „Naye, BWANA-arusi: anakuja, tokeni mwende kumlaki“ (Mt 25). Ujumbe halisi wa Neno unatangulia Kuja kwa Pili kwa Kristo.
Ujumbe wa mwisho ulichukuliwa tangu myaka mingi. Lakini Kuja kwake kutakuwa kwa gafla, kulingana na yale BWANA mwenyewe alisema: „Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hata magharibi, hivyo ndivyo kutakavyo kuwa kuja kwake kwa Mwana wa Adamu“ (Mt 24:27). Hiyo itafanyika kama vile kufumba na kufumbua: „…kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho; …na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika“ (1 Kor. 15:52).
Paulo ameeleza sana kwenye baruwa nyingi akionyesha namna gani mambo haya yatatendeka na vitu gani vitakavyo fanyika kwa wakati huo. Mitume wote walieleza kuhusu kuja kwa Pili kwa Kristo katika Baruwa zao. 1. Thes 5:23 mutume alimaliza akisema maratena kuhusu somo hiyo: „Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; ninyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama watika wa kuja kwa BWANA wetu Yesu Kristo!“
Kwa wakati mtu wa Mungu Willliam Branham alisema mara 1, 400 matayarisho ya bibiarusi wa Kristo kwa ajili ya unyakuo. Alifanya hivyo akiwa chini ya utume wa BWANA. Kupitia hudma ya kipekee yote yangelipashwa kwanza kurudishwa na kuwekwa kwa nafasi yake katika Kanisa. Hii ndiyo ahadi ya wakati wetu: „Naye akajibu, akawaambia, kweli Eliya yu aja kwanza, naye atatengeneza yote“ (Mt 17:11; Mk 9:12).
Wakati ya muhimu kwa mwisho wa wakati wa neema imekuwa sehemu ya utangazaji wangu kwa myaka mingi kupitia hudma yangu, pamoja na mafundisho yote ya kibiblia. Niliacha kila somo kwa hali ya kulingana na ginsi inavyo andikwa katika Biblia. Nimetupilia mbali kila matafsiri. Wakati umepita; ahadi ya kurudi (Jn 14) kwa BWANA na mkombozi ni karibu sana mkononi. Nikuhusu ujao wa kurudishwa wa musingi ya kibiblia kama vile matayarisho ndani ya imani na kutii kwa ajili ya siku ya utukufu wa Kristo (Flp 1:6).
Paulo, alie tangaza Neno kwa utume wa Kimungu aliwaamusha wa filipi na maneno haya „…Mkishika neno la uzima; nipate sababu ya ku furahi katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala siku jitaabisha bure.“ (Flp 2:16). Hivyo ndivyo nami ninavyo amsha sasa waamini wote wa Biblia, katika mataifa yote na lugha zote, kupitia utume wa kimungu.
Katika ufunuo 19:7; kundi la watu wengi walio nyakuliwa kutoka duniani wana imba: „Natufurahi, tukashsngilie tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya mwana kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari…“ Katika Mt 25:10 imeandikwa: „…Nao waliokuwa tayari, wakaingia naye arusini; mlango ukafungwa.’’
Tunaishi kwa wakati wa muhimu sana mbele ya kurudi kwa Kristo; hapo sasa inastahi semeka na kusemeka mara tena, ili waamini wote wa kiblia walisikie na kuliamini: Tarehe Juni, 11, 1933, kuna kitu cha ajabu kilicho tendeka: wakati muhubiri kijana William Branham alipo kuwa akibatiza waamini katika mto Ohio, kishindo lilitoka mbinguni na wingu kubwa la kimaajabu lenye nuru lilishuka, wazi wazi machoni pa watu wote walioku wa mahali pale. Hapo sauti lenye nguvu lili sikilika: “Kama vile Yohana mbatizaji alivyo tumwa kutangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo, Umetumwa na ujumbe ambao utatangulia kuja kwa pili kwa Kristo“. Ndugu Branham alilinganisha hii tukio hili la kimaajabu, katika mahubiri mengi tofauti mara 18. Aliweka mkazo kwa mba: “Si mimi mutangulizi, baali Ujumbe ndiyo utakao tangulia“.
Utume halisi na masomo nyingine ziligeuzwa na wale waabudu Branham huko Marekani, walipo andika yafwatayo: „Kama vile Yohana Mbatizaji alivyo tumwa kutangulia kuja kwa kwanza kwa Kristo, nawe unatumwa kutangulia kuja kwake kwa pili“.
Mtu alietumwa kutoka kwa Mungu alitangaza mafundisho yote ya kibiblia; kwa kweli alitangaza shahuri zote za Mungu ili kila kitu katika Kanisa la Yesu Kristo kirudi kwanafasi yake kamili. Ali sisitiza ya kwamba Mungu moja wa milele alijifunua yeye mwenyewe kwa ajili ya okovu wetu, kama vile Baba mbinguni katika Mwana wake mpendwa hapa duniani na kupitia Roho mtakatifu katika Kanisa lake. Mungu alikuwa katika Kristo akiuambatanisha ulimwengu pamoja naye (2. Kor 5:19, 1. Tim 3:16).
Ndugu Branham alihubiri Injili kwa Ujao, kama vile Petro na Paulo walivyo fanya kwa wakati wao. Alielewa vizuri kazi yake kubwa ya utume katika Mt 28:19 Ilikuwa ina husu Jina ya ubatizo, na moja Marko 16:16, mahali inayo husika na Imani, na katika Luka 24:47 mahali munapo semeka kuhusu usamaha wa dhambi. Ali hubiri msamaha wa dhambi kupitia damu ya Kristo iliyo tolewa, na alibatiza waamini kama vile Petro alivyo iagiza kwa mahubiri yake ya kwanza siku ya Pentecoste, kupitia chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. “Tubuni, na mukabatizwe kila mmoja wenu katika jina la Yesu Kristo kwa ondoleo la dhambi…“
Siku hiyo nafsi Elfu tatu ziliamini kupitia mahubiri yake ya kwanza chini ya umwangaji wa Roho mtakatifu, na walibatizwa (Matendo 2:14-41).
Katika Kanisa la kwanza wale wote walio amini, kati ya wayuda, wa samaria ao mataifa walibatizwa katika Jina la BWANA Yesu Kristo (Matendo 8:16; Matendo 10:48). Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji nao walibatizwa namna hiyo „Walipo sikia hayo, walibatizwa katika Jina la BWANA Yesu“ (Matendo 19:5). Ubatizo katika majina matatu ao chochote kama kile hakija kuweko katika Biblia, ilianzishwa na Athanase kwa karne ya nne.