'
Sura iliyotangulia

Nina wasaalimu kwa moyo wangu wote ndani ya jina la thamani la Yesu, kwa maana haya ya lsaya 54:14, 15, 17:

“Utathibitika katika haki. Utakuwa mbali na kuonewa, kwa maneno hutaogopa, na mbali na hofu, kwa maana haita kukaribia tazama, yamkini watakusanyana, lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakao kusanyana juu yako wataaguka kwa ajili yako. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakao inuka juu yako katika hukumu utauhukumiwa kuwa mkosa. Huu ndiyo urithi wa watumishi wa BWANA na haki yao inayotoka kwangu mimi, Asema BWANA”.

Tunapashwa kuwa na uhakika wa hii, ya kwamba Mungu anapigana kwa ajili yetu, kama tunasimama kwa upande wake. Tuna jikuta katikati ya vita vya kiroho; lakini BWANA amekwisha kushinda nguvu zote za yule adui. Hatupashwi wala kuogopa, wala kuwa na hofu kinyume ya ile tukiwa wenye kujawa na uhakika mwingi tunasema: “Kama Mungu yuko kwa upande wetu, ni nani atakaye kuwa juu yetu? Watu wanaweza kutufanya nini?.” Hakuna silaha hata moja iliyo fanyika juu ya watu wa Mungu itakayo fanikiwa kuwa gusa, na kila ulimi utatao jiinua juu ya wateule utahakikishwa kuwa ni wauwongo. Huu ndiyo urithi wa yule amwaminiye Mungu kwa moyo wote na anaye mtumainia yeye.

Sura inayofuata